Tuesday, 12 August 2014

WANACHI WA KWA MOROMBO WAPO HATARNI KUPATWA NA MAGONJWA YA MILIPUKO


 Hili ni moja ya dimbwi lililopo katika makaazi ya watu lenye maji machafu (Picha na Charles Chami)

Wananchi wa eneo la kwa morombo mkoani arusha wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya milipuko kutokana na uchafu wa mazingira katika maeneo hayo

Maeneo hayo ya kwa morombo wananchi wamekuwa wakiishi katika mazingira machafu na hatarishi uku wengine wakikiri kupatwa na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu, kichocho na kuhara damu
Melina Lengidale ni moja wa mkaazi wa kata ya terati eneo la kwa morombo ambapo amesema tatizo hili limekuwa la muda mrefu bila kufanyiwa ufumbuzi wa aina yeyote
Aidha ameeleza viongozi wanaoingia madarakani wamekuwa wakihaidi kutatua tatizo hilo  ama changamoto hizo hii ambayo imekuwa kero kubwa kwa wanaanchi lakini waingiapo madarakani hushindwa kutimiza ahadi zao
“viongozi wote hii ni kama hawamu ya pili kila uongozi ukiingia madarakani wala hata hawasimamii swala hili sio la maji wala barabara wote wanatuacha njia panda”


Kulia mmoja wa wafanya biashara katika eneo hilo la kwa morombo Bi Florida ngonyani  akifanya maojiano na mwandishi wetu  Janeth Sisso  jana (picha na Charles Chami)
Hata hivyo viongozi wa eneo hilo la kwa morombo akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Frances Mbise amekiri kuwepo na tatizo hilo na kuhaidi kulifanyia kazi tatizo hilo   Habari na Janeth sisso

No comments:

Post a Comment