Tuesday, 12 August 2014

UVIVU NI ADUI WA MAENDELEO

Fundi mitando bw.Aziz Mwinuka akitoa ufafanuzi juu ya mambo yanayoikabili studio za Ajtc Radio huku mwandishi wa Ajtc Bi.Lilian Deus( Picha na Nurdin Pallangyo)
Na.LILIAN DEUS.
Wanafunzi  wa  chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) wameaswa kutumi muda wao kufanya mazoezi kwa vitendo ya uandishi wa habari na kutangaza na kuandaa vipindi tofauti vya Radio ili wawaze kujijenga na kuwa wazuri katika tansia hii ya uandishi.

Rai hiyo imetokewa na mmoja wa viongozi wa studio katika chuo hicho ambaye pia ni fundi mitambo mkuu wa Radio AJTC Bw.Aziz Mwinuka wakati akizungumza na mwandishi wa Ajtc  Radio.
Amesema wanafunzi wengi wamekuwa wavivu katika suala zima la kutangaza na kuandaa vipindi vya Radio jambo ambalo limekuwa kama ni mazoea yao

Pia bw.Mwinuka amesema kuwa studio yao inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kisasa( digitali) kama vile vipaza sauti yaani microphones na Mixer lakini kutokuwa na uwepo wa vifaa hivyo hakukwamishi shughuli za studio.

No comments:

Post a Comment