Wednesday, 13 August 2014

HABARI KIMATAIFA : Mtuhumiwa azua kihoja mahakamani Rwanda

Rwanda imekuwa ikiendedesha harakati za upatanishi na pia kuwakumbuka waliokufa katika mauaji hayo


Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Emmanuel Mbarushimana amekataa uendeshwaji wa kesi yake na mahakama ya Kigali kwa kutoa pingamizi kwamba hana haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.


Mshukiwa huyo alikabidhiwa Rwanda na nchi ya Denmark mapema mwezi wa saba mwaka huu ili kujibu mashitaka ya kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.


Mushukiwa huyo Bwana Emmanuel Mbarushimana amesema kesi yake haiwezi kusikizwa hadi pale atakapopata haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.


Hoja yake ilikuwa kwamba ni lazima na yeye aruhusiwe kukaa badala ya kusimama wakati kesi yake ikisikilizwa na wakati huo huo mwendesha mashitaka asimame badala ya kukaa kama ilivyozoeleka.


Aidha, amesema kuwa hajafurahia utaratibu unaotumiwa wa kuingia katika chumba cha mahakama ambapo mwendesha mashitaka na majaji wanaingia kwa kutumia mlango mmoja kinyume na mushitakiwa.


Mwendesha mashitaka amemshitaki kwa kushiriki katika mauaji dhidi ya watutsi yaliyotokea katika maeneo mbali mbali katika mkoa wa zamani wa Butare kusini mwa Rwanda.
Mushukiwa pia ameleta hoja nyingine ya kwamba hana wakili.
Swala hilo la kuwa na wakili lilikuwa limeshajadiliwa katika kikao cha kesi kilichotangulia ambapo alipewa muda wa kuchagua wakili anayetaka.


Wakati huo alipewa orodha ya mawakili 500 miongoni mwa mawakili wanaohudumu hapa nchini na kuikataa.
Alipendekeza kupewa orordha nzima ya mawakili wote kwa ujumla ili amchague mmoja anayetaka.Kipindi alichokuwa amepewa kuchagua wakili huyo kilikuwa kimemalizika.


Mahakama imesema kuwa hoja hizo haziwezi kuzuiya kesi hasa ikiwa ni kesi ya kukiri ama kukana mashtaka dhidi yake;jambo alilokataa kata kata akisema mahakama haina uhuru wala haki.


Imetangazwa kuwa Uamuzi kuhusu mabishano hayo utatolewa kesho.


Emanuel Mbarushimana mwenye umri wa miaka 50 alikabidhiwa Rwanda na mahakama ya Denmark mapema mwezi uliopita ili kujibu tuhuma za kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.::
Chanzo Cha habari hii BBC SWAHILIHABARI  /  NA  AGAPE MSUMARI

MICHEZO || AJTC STARS KATIKA UZI MPYA PICHA KAMILI ZIKO HAPA

Chama cha waandishi  wa habari za michezo Tanzania kimetimiza ahadi yake ya kutoa jezi kwa chuo cha uandishi wa hababari na utangazaji arusha (AJTC) .
Ahadi hiyo  ni kufuatia ushindi walioupata katika bonanza la vyombo vya habari na utatangazaji  kanda ya kaskazini.





HABARI  NA PICHA  :: AGAPE MSUMARI

WANAFUNZI FUNGUENI BLOG

Nurdin Pallangyo (kulia)wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha alitoa maelezo juu ya wanafunzi wa AJTC kufungua blog kushoto ni mwandishi wa blog Udzungwa class Grace Frank.(Picha na Johaness Johnson)

NA.GRACE FRANK.
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wameshauriwa kufungua blog ili kuendeleza vipaji vyao.

MITINDO || TAZAMA PICHA ZA JINSI YAKUWEKA POZI TOFAUTI KWA KINA DADA WAKATI WAKUPIGA PICHA NZURI

 Kwa kina dada wale  ambao wanapenda kuonekana vizuri katika picha mbali mbali hii hapa ni muhimu kwao kujifunza namna yakukaa wakati unapiga pichazako 
                                                     TAZAMA PICHA HIZO HIZI HAPA








 HABARI NA JIMMY MINJA 

Tuesday, 12 August 2014

POLISI LIBYA AUAWA


HABARI NA GRACE FRANK.
Mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Libya Tripoli, ameuawa na watu wasiojulikana.

TATIZO LA WANAFUNZI WA AJTC KUHAMA NA KWENDA KUPANGA


Mkufuzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Adson Kagiye akihojiwa na mwandishi wa AJTC Radio Jesca Willy kuhusu wanafunzi wanaohama Hostel na kwenda kupanga vyumba.(Picha na Johaness Johnson)

HABARI NA JESCA WILLY

Wanafunzi  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Arusha,  wanaoishi  nje  ya   hostel, wameshauriwa    kufuata  sheria  za  nchi, nakufuata  kilicho  weleta chuoni   hapo  ili  kutimiza  malengo  waliyo  jiwekea  katika  katika maisha yao.

HABARI KIMATAIFA || Polisi wa Misri watuhumiwa kwa mauaji


Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema kwamba vikosi vya askari wa Misri viliua idadi kubwa sana ya wananchi kuwahi kushuhudiwa ndani ya siku moja mwezi Agosti mwaka jana.

 Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani. Kwa muujibu wa taarifa zilizotolewa na kikundi hicho cha utetezi wa haki za binaadamu zinaeleza kwamba mauaji hayo ya waandamanaji waliokuwa wanampinga Raisi Mohammed Morsi,raia wapatao mia nane waliuawa katika uwanja wa Rab'a mjini Cairo mnamo tarehe 14 mwezi August mwaka 2013.

Kadhalika shirika hilo la kutetea haki za binadamu linasema kwamba mauaji hayo ya raia ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu na kuwataka viongozi wenye dhamana wa Misri kutenda haki juu ya maisha ya raia hao.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa shirika hilo, Kenneth Roth ambaye alizuiliwa kuingia ndani ya nchi ya Misri mapema wiki hii na kueleza alichokishuhudia na kuyafananisha na mauaji hayo na yale yaliyowahi kutokea katika uwanja wa Tiananmen nchini China.Chanzo BBC :: Habari Na Jimmy Minja