Twaha Yahaya mkazi wa Olasit akitupa taka katika eneo la barabara iliyopo karibu na makazi ya watu.(Picha na Grace Mboya.)
NA;
Grace Mboya,
ARUSHA.
Wananchi wa kata ya
olasiti iliyopo Mkoani Arusha wameulalamikia uongozi wa vijiji vyake kwa
kutokuweka utaratibu mzuri wa utunzaji wa mazingira.
Malalamiko hayo yametolewa hivi karibuni na baadhi ya wakazi wa eneo
hilo baada ya kufanya mazungumzo na mwandishi wetu kuhusiana na kuzagaa kwa
uchafu unaonekana kuwa kero bembezoni mwa barabara za kata hiyo.
Hali ya mazingira ya kijiji cha Olast inavyoonekana kuwa atarishi kwa afya za wananchi wa eneo hilo.(Picha na Grace Mboya)
Walisema kuwa
awali walikuwa na utaratibu wa kuzikusanya taka hizo bembezoni mwa barabara
katika maeneo yaliyotengwa kwa siku tofautitofauti kulingana na mgao wa vijiji na gari linafika kwa siku hiyohiyo
kuzibeba na kuzipeleka katika jalala kuu la manispaa.
“Yaani
mwanzoni tulikuwa na utaratibu mzuri wa kuzikusanya hizi takataka na huwezi
kuona hali chafu kama unayoiona ila kwa sasa atuelewi maana gari tuna muda sana
atujaliona”.Alisema Hadija Yahaya mkazi wa eneo hilo.
Pia
walieleza hofu yao kuhusiana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababishwa na
mazingira hayo yasiyo rafiki kwa afya zao kwani vituo hivyo vipo jirani na
makazi ya watu na kuomba uongozi kuweka
utaratibu mpya kama huo wa awali umeshindikana.
Mwandishi wetu Grace Mboya akifanya mazungumzo na Elia Kambai mkazi wa Olasiti kuhusiana na hali ya mazingira katika kijiji hicho.(Picha na mpiga picha wetu.)
Kwa upande wa baadhi ya wapangaji wa kata hiyo
walisema kwao hiyo ni fursa kwani watazichoma taka hizo ili kuepuka kutozwa
kiwango cha juu cha fedha ambacho wanatozwa kwa sasa.
“Tulikubaliana
kuwa sisi wapangaji tunatakiwa kulipa elfu moja na wenye nyumba za familia
wanalipa elfu tatu pamoja na wenye vituo vya biashara lakini kwa sasa wapangaji
tunaambiwa tulipe elfu moja mia tano heri tu hilo gari lisije tutazichoma
wenyewe”.alieleza John Peter mpangaji wa eneo hilo.
Juhudi za
kumtafuta kiongozi wa kijiji cha olasiti hazikuzaa matunda baada ya kufika
katika ofisi yake na kukuta imefungwa na kutokupatikana kwenye namba yake ya
simu.
No comments:
Post a Comment