Tuesday, 12 August 2014

TATIZO LA WANAFUNZI WA AJTC KUHAMA NA KWENDA KUPANGA


Mkufuzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Adson Kagiye akihojiwa na mwandishi wa AJTC Radio Jesca Willy kuhusu wanafunzi wanaohama Hostel na kwenda kupanga vyumba.(Picha na Johaness Johnson)

HABARI NA JESCA WILLY

Wanafunzi  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Arusha,  wanaoishi  nje  ya   hostel, wameshauriwa    kufuata  sheria  za  nchi, nakufuata  kilicho  weleta chuoni   hapo  ili  kutimiza  malengo  waliyo  jiwekea  katika  katika maisha yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha,  Bw.Adison Kagiye, alipokuwa anahojiwa na Ajtc redio nje ya ofisi yake hapo jana .
Bw.Adison Kagiye amesema kuwa, chanzo cha kuhama kwa wanafunzi hao ni kutokana na kukosa uhuru, kusikiliza maneno ya watu, na kushindwa kulipa gharama za hostel,  hivyo  kupelekea  kuhama ili kuepuka matatizo hayo yanayo wakabili.
Mkufunzi huyo mefafanua zaidi kwakusema kuwa,  wanafunzi wana maamuzi yakuchagua sehemu wanayo taka kuishi  wao wenyewe, bila kupangiwa na mtu yeyote ,kwani nao ni  raia kama wengine wanao ishi kwa kujitegemea
Bw. Adsoni ameongeza kwakusema, zipo changamoto mbalimbali zinazo wakabili kwa kuama kwa wanafunzi, mojawapo ikiwa ni kukosa fedha, wengine kutoweza kumaliza fedha wanazo daiwa pia hata kuchomwa visu kwa wanafunzi wanao ishi nje ya hostel ni moja ya changamoto wanazokumbana nazo.
Mkufunzi huyo bw. Adson kagiye amemalizia kwa kusema kuwa, wanafunzi wote wanaokaa nje na ndani ya hostel ,wanatakiwa wasome ili kuepuka kufeli katika masomo yao, kwani kufeli kunachangiwa na wote wanao kaa nje na ndani ya hostel. 


No comments:

Post a Comment