Shirika la
kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema kwamba vikosi vya
askari wa Misri viliua idadi kubwa sana ya wananchi kuwahi kushuhudiwa ndani ya
siku moja mwezi Agosti mwaka jana.
Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi
kushuhudiwa duniani. Kwa muujibu wa taarifa zilizotolewa na kikundi hicho cha
utetezi wa haki za binaadamu zinaeleza kwamba mauaji hayo ya waandamanaji
waliokuwa wanampinga Raisi Mohammed Morsi,raia wapatao mia nane waliuawa katika
uwanja wa Rab'a mjini Cairo mnamo tarehe 14 mwezi August mwaka 2013.
Kadhalika
shirika hilo la kutetea haki za binadamu linasema kwamba mauaji hayo ya raia ni
uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu na kuwataka viongozi wenye dhamana wa Misri
kutenda haki juu ya maisha ya raia hao.
Hayo yamesemwa
na kiongozi wa shirika hilo, Kenneth Roth ambaye alizuiliwa kuingia ndani ya
nchi ya Misri mapema wiki hii na kueleza alichokishuhudia na kuyafananisha na
mauaji hayo na yale yaliyowahi kutokea katika uwanja wa Tiananmen nchini China.Chanzo BBC :: Habari Na Jimmy Minja
No comments:
Post a Comment