
Na Janeth Sisso
Ulinzi katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayofanyika katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere umeimarishwa na kazi ya kufunga kamera za ulinzi imekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe alisema amelazimika kufanya ziara hiyo ili kukagua hali ya usalama katika eneo hilo.
“Kimsingi nimekuja kukagua hali ya usalama uwanjani hapa. Unajua maonyesho haya yanajumuisha watu kutoka mataifa tofauti na sisi tumelazimika kujipanga ili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na ndio maana kuna ukaguzi milangoni,” alisema.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu aliwataka watu kuheshimu utaratibu wa ukaguzi uliowekwa na wale ambao wanamiliki silaha hawataruhusiwa kuingia nazo.
No comments:
Post a Comment