Mabingwa katika
mpira wa miguu na mpira wa Pete(Netball)Chuo cha Arusha Journalism Training
College(AJTC)wakishangilia ushindi wao.
![]() |
| wanafunzi wa AJTC Mabingwa katika mpira wa miguu na mpira wa Pete(Netball)Chuo cha Arusha Journalism Training College(AJTC)wakishangilia ushindi wao. |
a
Arusha.Timu ya soka na ya mpira wa pete za Chuo Cha Uandishi
wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la
waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini.
Katika bonanza hilo, lilifanyika katika uwanja wa Sheikh
Amri Abeid kwa kuandaliwa na Taswa Arusha na kampuni ya Ms Unique, jumla ya
timu 10 zilishiriki kutoka mkoa wa Arusha na Manyara.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa
mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo,
waliwashinda timu ya chuo cha uandishi
wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5. SOMA ZAIDI
Mgeni rasmi katika bonanza Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma
Pinto alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa very soka alipewa
kikombe, ,fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Huku mshindi wa pili soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa
mpira wa pete alizawadiwa kikombe cha fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa
pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia
nchini, (Tbl), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro,
Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel timu
nyingine zilizoshiriki ni Radio 5.
Nyingine ni timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara,
Salam Club, IMS na Taswa Arusha Arusha
ambayo iliambulia ushindi katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi
na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi the nzuri waliofanya.
Pinto pia aliahidi katika maadhimidho ya miaka 10 ya bonanza
hilo, mkutano mkuu wa T aswa Taifa utafanyik a Arusha sambamba na tuzo za
waandishi bora.
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi Tbl
kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi
wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza
wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kue
kudhamini.

No comments:
Post a Comment