Thursday, 3 July 2014

MASHINDANO YA UTANGAZAJI AJTC KUWAKA MOTO!



Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji cha jijini Arusha kimetangaza rasmi mashindano ya utangazaji kwa wanafunzi wote chuoni hapo.


Akitoa taarifa hiyo mkuu wa idara ya utangazaji kwa wanafunzi hao bwana onesmo mbise alisema mshindi wa mwaka huu atazawadiwa kombe na fedha taslim shilingi elf 60, wakati mshindi wa pili atapata shilingi elf 50 na mshindi wa tatu atajinyakulia kreti mbili za soda.
Aidha bwana mbise aliwataka wanafunzi hao kutumia muda uliobakia kujiandaa vilivyo na mashindano hayo
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa wiki moja kuanzia tarehe 21 mpaka 25 julai.
HABARI NA AGAPE MSUMARI.

No comments:

Post a Comment